Swahili   |   English
Usajili wa Vizazi

Usajili wa vizazi unasimamiwa na sheria ya uandikishaji vizazi na vifo,(sura 108 toleo la 2002)

Kulingana na sheria kizazi inatakiwa kuandikishwa ndani ya siku 90 tangu kutokea kwake na kifo ndani ya siku30,na Tukio hilo Lazima liwe limetokea ndani ya mipaka ya Tanzania Bara.Pamoja na takwa hili sheria inaruhusu usajili kufanyika nje ya muda huu.Wajibu wa kusajili kizazi ni kama ufuatao:

NB: Baba au Mama,na kama Baba na Mama hawapo,mmiliki wa nyumba ambaye ana taarifa za kizazi kutokea,mtu yoyote ambaye amekuwapo wakati kizazi kikitokea au mtu yoyote ambaye mtoto aliyezaliwa yuko katika himaya yake.

 

UTARATIBU WA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA

1: Usajili wa kizazi ndani ya siku 90

  • Kama kizazi kimetokea hospitalini,kituo cha afya au zahanati hakikisha unapatiwa Tangazo la kizazi kabla ya kuondoka.
  • Endapo kizazi kitakuwa kimetokea nyumbani,toa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa kijiji au Msajili wa vizazi au vifo wa wilaya ili ipatiwe tanzazo la kizazi.taarifa hii itolewe ndani ya siku 90.
  • Wasilisha tangazo la kizazi kwa msajili wa vizazi na vifo wa wilaya kilipotokea kizazi
  • Lipa ada ya cheti inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 8,000/=).

 

2: Usajili nje ya siku 90 lakini chini ya miaka 10.

  • Jaza na wasilisha Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3  (ijazwe na mzazi au mlezi)
  • Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
  • Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono maelezo yako kwenye fomu.nyaraka hizi ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
  • Lipia ada inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi  8,000/=)

3: Kuandikisha kizazi kilichochelewa kuandikishwa zaidi ya miaka 10

  • Jaza na wasilisha  Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3 (ijazwe na mzazi au mlezi).
  • Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
  • Ambatanisha nyaraka ,kadi ya kliniki ya mtoto,cheti cha ubatizo kamakipo,barua kutoka mamlaka ya serikali zinazohusika kama vile ofisi ya mtendaji kata au kijiji),cheti cha kumaliza elimu ya msingi, cheti cha kumaliza elimu ya sekondari  kuthibitisha tarehe ya kuzaliwa,mahali pa kuzaliwa na uraia wa wazazi.
  • Kwa watu walio zaliwa zamani sana unapaswa kuwa na viambatanisho viwili ambapo utatakiwa kuwa na kadi ya utaifa pamoja naya kura au bima ya afya, kama mwombaji anataka kutumia kadi ya leseni ya gari lazima iambatane pamoja na kadi ya utaifa au ya kura.
  • Lipa ada  shilingi 20,000/= 

4: Kupata nakala ya cheti baada ya kupoteza.

  • Wasilisha ombi lako ukionesha namba ya ingizo jina la mwenye cheti,mahali pa kuzaliwa na tarehe ya

           kusajiliwa.

  • Jaza taarifa zako katika Fomu ya kutafutia kumbukumbu (search form)
  • Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tsh. 7,000)

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa

  • Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa
  • Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako – barua inayotetea ombi lako na kiambatanisho(cheti cha ubatizo,kadi ya clinic au vyeti vya shule na vielelezo vingine msajili atakavyohitaji kwaajili ya kujiridhisha, vielelezo vya wazazi kama vile cheti cha kuzaliwa, vyeti vya vifo au vitambulisho vyao  ikiwa jina la mmoja wa wazazi limekoseewa)
  • Rejesha cheti kinachotakiwa kusahihishwa.
  • Ada baada ya ombi lako kukubaliwa (ada ya sasa ni Tsh 13,000/= )

                 

TANBIHI

  1. Kubadili au kuongeza jina.
    Sheria inaruhusu kubadili au kuongeza jina ndani ya miaka miwili tangu tarehe ya kusajiliwa.Baada ya muda huu kupita daftari la kizazi haliwezi kurekebishwa kwa badiliko la jina,mhusika atatakiwa kufuata utaratibu mwingine chini ya sheria ya kubadili jina kwa ajili ya (Deed polls).
  2. Taratibu mpya za kupata vyeti vya kuzaliwa kwa walio nje ya nchi.soma zaidi

>>> MASWALI MBALI MBALI YANAULIZWA KUHUSU VIZAZI