Swahili   |   English
Usajili wa Ndoa

USAJILI WA NDOA 

RITA husajili Ndoa na Talaka, na pia hutoa vyeti. Usajili wa Ndoa na Talaka unaongozwa na Sheria ya Ndoa ya 1971 Sura ya 29 toleo la 2002.

  1. 1.    Kusajili ndoa inayodumu iliyokuwa haijasajiliwa

Mahitaji/Taratibu:

  • Jaza fomu zinazohusika (RGM 18RGMF 7).
  • Hati ya kiapo cha Ndoa (Ionyeshe kuwa Ndoa inadumu na haijasajiliwa).
  • Ambatisha nakala za vyeti vya uzazi wa watoto wa ndoa kama wapo.
  • Ambatisha Ushahidi kuthibitisha ndoa yako. Mfano:- Cheti kilichotolewa na Kiongozi wa dini nk.
  • Lipa ada halisi (ada ya sasa ni Tsh. 20000/=.

 

  1. 2.    Kupata cheti cha kutokuwa na kizuizi cha ndoa

Mahitaji/Taratibu

  • Jaza na wasilisha Fomu RGM 12.
  • Wasilisha nakala za cheti cha kuzaliwa na pasipoti.
  • Idhini ya maandishi ya mzazi/mlezi kuthibitisha kuwa mwombaji hana ndoa.
  • Kitambulisho cha mzazi au mlezi aliyeidhinisha kuwa mwombaji hana ndoa.
  • Lipa ada sahihi Tsh. 200,000/=.
  • Fomu inapaswa kuombwa na mwombaji.

Tanbihi: Iwapo muombaji anaishi ng'ambo, maombi yapitie Ubalozi wa Tanzania au Ubalozi mdogo katika nchi anayoishi.

 

  1. 3 Maombi ya leseni ya kufungisha ndoa

Taratibu

  • Jaza form  RGMF 2 
  •  Mwombaji ambaye ni mara yake ya kwanza atatakiwa aambatishe barua ya utambulisho toka kwa kiongozi wake, cheti cha usajili wa taasisi na picha mbili aina ya passport size.
  • Kama ni maombi ya kuhuisha leseni, ambatisha leseni yako ambayo muda wake umeisha pamoja na picha yako moja ya passport size.
  • Lipa ada ya maombi ya Tsh 30,000/=
Tanbihi: Mkuu wa Taasisi ya Dini husika anapaswa kujaza form ya RGMF 2 (Endapo utajiombea mwenyewe, itakulazimu maombi yako yapitie kwa Mkuu wa Wilaya yako, ambaye atatoa maoni kuhusu ombi lako).

  1. 4 Kupata kibali cha kufunga ndoa ndani ya siku 7.

Mahitaji/Taratibu

  • Jaza Fomu RGMF. 9 
  • Thibitisha kimaandishi sababu za kutosha kwanini notisi ya siku 21 isitolewe.
  • Uwepo halisi wa wanandoa.
  • Wasilisha utambulisho wa wanandoa (pasipoti, kitambulisho cha kazi n.k)
  • Picha moja moja ya passport size
  • Kwa mgeni kutoka nje ya nchi anatakiwa awe na uthibitisho wa kutokuwa na ndoa toka nchini kwake au ubalozini.
  • Lipa ada halisi ambayo ni Tsh 100,000

 

  1. 5.    Kibali cha kufunga ndoa mahali maalum

RITA (Msajili Mkuu) hutoa kibali maalumu cha kufunga ndoa mahali maalumu, zaidi ya mahali palipozoeleka kutumika kwa ibada au mikusanyiko.


Mahitaji/Taratibu

  • Jaza Fomu RGM. 4
  • Toa sababu kwanini unataka kufunga ndoa katika sehemu ile na si mahali palipozoeleka.
  • Fomu hiyo isainiwe na kugongwa muhuri na mfungishaji ndoa (Katibu Tawala wa Wilaya au Kiongozi wa dini)
  • Lipa ada inayohusika Tsh.200,000/=.
  • Ada kwa mgonjwa  ni  Tsh 20,000/=

 

  1. 6.    Kusajili ndoa iliyofungwa nje ya nchi

RITA (Msajili Mkuu) husajili ndoa zilizofungwa nje ya nchi.


Mahitaji/Taratibu

  • Jaza Fomu RGMF 7 na RGM. 11.
  • Ambatisha nakala ya Kiingereza au Kiswahili ya cheti chako cha ndoa (iwapo cheti chako cha ndoa hakiko katika Kiingereza au Kiswahili cheti kilichotafsiriwa na ofisa anayehusika au mthibitishaji wa umma.
  • Ambatisha kopi ya pasi ya kusafiria ya wanandoa.
  • Ambatisha nakala mbili za pasport size
  • Lipa ada inayotakiwa, kwa sasa ni Tsh. 100,000/=. 

  • TANBIHI: Ndoa iliyofungwa katika balozi za Tanzania za ng’ambo zinachukuliwa kama ndoa zilizofungwa Tanzania bara ambazo hazikufuata utaratibu huu.

>>> MASWALI MBALI MBALI YAYOULIZWA NA MAJIBU YAKE