Swahili   |   English

CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO

CHA WAKALA WA USAJILI UFILISI NA UDHAMINI(RITA SACCOS LTD)

KUHUSU/HISTORIA YA RITA SACCOS

RITA SACCOS LTD ni ushirika uliosajiliwa kwa ajili ya kutoa  huduma ya  Mikopo  kwa wafanyakzi walioajiriwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA).

RITA  SACCOS LTD ilianzishwa mwaka 2010 na imesajiliwa rasmi katika chama cha ushirika. SACCOS ilianzishwa na wanachama hai 24 , lakini sasa idadi ya wanachama wa RITA SACCOS LTD inaongezeka na kufikia hadi 90.

Lengo la Saccos  ni  kuhamasisha akiba kutoka kwa wanachama na kwa kurudi kutoa huduma za mikopo. Malengo mengine ya RITA SACCOS LTD ni kuhamasisha wanachama wake kwa kufundisha wanachama manufaa ya kuendeleza  tabia ya akiba, kupitia njia nzuri za uwekezaji bora ili kuboresha hali ya kijamii na kiuchumi ya wanachama.

Ofisi ya RITA SACCOS  ziko katika ofisi ya Makao Makuu ya RITA,Floor ya 4 , Dar es Salaam.

MAWASILIANO:

Simu Mwenyekiti: +255784216490

 

RITA SACCOSS

Box 9183,

DAR ES SALAAM.

ritasaccos@rita.go.tz

 

TARATIBU MBALIMBALI ZA RITA SACCOS.

 

KUJIUNGA UANACHAMA

  1. Lazima awe Mwajiriwa wa RITA
  2. Ajaze fomu ya KUOMBA kujiunga na RITA Saccoss.(imeambatanishwa link ya fomu RITASACCOS1)
  3. Anapaswa kulipa Ada ya kiingilio
  4. Jaza fomu no TUF6 (Employment and Labour Relations) ya makato kwa mshahara wako
  5. Picha 2 kwa ajili ya kuweka kwa kitambulisho na kumbukumbu za Mwanachama wa Saccos
  6. Maombi yawasilishwe RITA Makao makuu , ofisi ya Saccos ama kwa njia ya Posta.
  7. Maombi yaambatane na malipo kwa uthibitisho wa  slip ya bank(Malipo yote yalipwe kupitia bank ya RITA SACCOS LTD)

KUOMBA MKOPO

  1. Mkopaji lazima awe mwanachama wa RITA SACCOS LTD
  2. Ajaze fomu ya MAOMBI YA MKOPO ya RITA SACCOS LTD (imeambatanishwa kwa link ya fomu RITASACCOS2)
  3. Jaza fomu no TUF6 (Employment and Labour Relations) ya makato kwa mshahara wako kulingana na mkopo.
  4. Aweke kuanzia HISA 5
  5. Ada ya Mwezi 6
  6. Maombi yawasilishwe RITA Makao makuu , ofisi ya Saccos ama kwa njia ya Posta
  7. Maombi yaambatane na malipo kwa uthibitisho wa  slip ya bank(Malipo yote yalipwe kupitia bank ya RITA SACCOS LTD)

ZINGATIA: MALIPO YOTE YANAPOKELEWA KWA ACCOUNT YA RITA SACCOS KWENYE TAWI LA CRDB, ACCOUNT NO 0150205200100. NA SI VINGINEVYO.