Fomu za kuombea leseni ya kufungisha ndoa zinapatikana

Taasisi za kidini ama watu binafsi kwenye madhehebu tofauti ya kidini kama mashehe, maimamu, mapadri na wachungaji wanaweza kupata fomu za kuombea leseni za kufungishia ndoa moja kwa moja kutoka kwenye tovuti yetu. Fomu za kuombea leseni za kufungishia ndoa zinapatikana katika tovuti yetu.

RGMF2 ni fomu ambayo muhusika anajaziwa na taasisi yake ili kumwezesha aweze kufunga ndoa.

    Unachotakiwa kufanya ni :-
  • Pakua fomu RGMF2
  • Jaza fomu 
  • Ambatanisha fomu na picha za passport mbili (2) kwa anayeomba leseni mpya, au picha moja (1) kwa anaye ongeza muda wa leseni.
  • Sahihi ya muombaji na mkuu wa wilaya
  • Muhuri wa taasisi
  • Ada shilingi elfu tano (sh 5,500)

    RGMF3 ni fomu ambayo muombaji anajaza mwenyewe ili kumwezesha kufunga ndoa.

    Unachotakiwa kufanya ni :-
  • Pakua fomu RGMF3 
  • Jaza fomu
  • Ambatanisha fomu na picha za passport mbili (2) kwa anayeomba leseni mpya, au picha moja (1) kwa anayeongeza muda wa leseni.
  • Sahihi ya muombaji
  • Ada shilingi elfu tano (sh 5,500).

Baada ya fomu kukamilika na viambatanisho vilivotajwa, inarudishwa kwenye ofisi za RITA makao makuu, Upanga Mtaa wa Kipalapala, nyumba namba 514.

Rita Internal Search

Matangazo
Video / Picha
Sheria



Events Calendar
September 2010
SunMonTueWedThuFriSat
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930