Swahili   |   English




Mkutano wa wadau kuhusu usajili na ukusanyaji wa takwimu za matukio muhimu ya maisha ya Mwanadamu
Date: 22 September, 2015 Author: Jafari Malema

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Maimuna Tarishi akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Usajili na Takwimu za Matukio muhimu ya Binadamu jijini Dare es salaam.

KATIBU MKUU WA WIZARA  YA KATIBA NA SHERIA BI. MAIMUNA TARISHI AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUJADILI MKAKATI WA KITAIFA WA USAJILI NA TAKWIMU ZA MATUKIO MUHIMU ( CIVIL REGISTRATION AND VITA STATISTICS – CRVS) JIJINI DAR ES SALAAM.

 

Rasimu Mkakati wa kitaifa wa Usajili na Upatikanaji wa Takwimu za Matukio muhimu jana iliwasilishwa na kujadiliwa na wadau wa Masuala ya Usajili katika Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya New Africa, Jijini Dar es Salaam.

Akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Maimuna Tarishi amewataka wadau wote waungane na kufanya kazi pamoja katika utekelezaji wa Mkakati huu. Pia aliwahakikishia Wadau kwamba Serikali itaendelea kushiriki na kufuatilia kwa karibu katika kuhakikisha malengo ya Mkakati huu yanafikiwa kwa wakati.

Matukio muhimu kwa Mwanadamu ni Vizazi, vifo na sababu zake ndoa na Talaka . Mkakati huu una lengo la kuboresha mifumo yote inayotumika kusajili matukio haya ili kuwa na mfumo utakaowezesha matukio haya kuweza  kusajiliwa mara yanapotokea na takwimu sahihi kuweza kupatikana kwa wakati.

Wadau walioshiriki ni pamoja na kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wadau wa Maendeleo na watumishi wa Idara mbalimbali za Serikali.