Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Picha za Albamu
Album:           KAMPENI YA WOSIA MBEYA

Description: Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya Bi Quip Mbeyela ambaye ni Mgeni rasmi akiwahutubia Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu na huduma ya msaada wa kisheria bure kuhusu kuandika na kuhifadhi Wosia na mambo ya Mirathi hii leo katika viwanja vya stendi ya Kabwe Jijini Mbeya kulia kwake ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la mbeya Bw Vicent Msolla na wengine ni Mawakili wa serikali kutoka RITA Makao Makuu. RITA inaendelea na kampeni kama hizi katika Wilaya mbalimbali nchi nzima kuhakikisha wananchi wanafahamu umuhimu wa kuandika na kuhifadhi Wosia na kushughulikia mambo ya mirathi ambapo eneo hilo limeonekana kuwa na migogoro mingi inayopelekea familia nyingi kukosa haki ya kurithi mali alizoziacha Marehemu na hivyo kusababisha Watoto kuacha shule na kukimbilia mitaani pamoja na Wajane kuanza maisha mapya ya umasikini na majuto.

Album Pictures