Description:
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA, umetoa maagizo kwa Wakuu wa Mkoa, Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na wataalam kutoka idara mbalimbali katika mkoa wa Dodoma na Singida wakati wa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo viongozi wa mikoa hiyo,iliyofanyika tarehe 28 Februari 2019. Semina hiyo ilihusu suala la kujipanga ili kutekeleza Mpango wa Kusajili na Kutoa vyeti vya kuzaliwa bila malipo kwa watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano unaotarajiwa kutekelezwa mwanzoni mwa mwezi Machi 2019.