Swahili   |   English
Gallery : Photo
Album:           RITA YAPOKEA UGENI

Description: RITA YAPOKEA UGENI KUTOKA ETHIOPIA NA SIERA LEONE KWA ZIARA YA MAFUNZO KUHUSU USAJILI WA VIZAZI Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) imepokea ugeni watu 16 kutoka nchi za Ethiopia na Siera Leone waliokuja kwa ziara ya Mafunzo katika maeneo ya Usajili wa Vizazi, utambuzi na Takwimu ambao watakuwa hapa nchini kwa ziara ya siku nne. Lengo la ziara hii ni kujifunza na kupata uzoefu wa jinsi Tanzania ilivyoweza kuleta mageuzi makubwa katika Usajili wa vizazi kupitia Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano unaotekelezwa nchini. Aidha, watapata maelezo ya kina ya jinsi Simu za Kiganjani zilivyoweza kutumika kutuma taarifa za watoto waliosajiiwa kwenda kwenye kanzidata ya Wakala. Mpaka sasa Mpango huo unatekelezwa katika Mikoa 23 ya Tanzania Bara na umewezesha zaidi ya watoto milioni 8.1 kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa Mpango huu unatekelezwa kwa kusogeza huduma za usajili karibu na wananchi hivyo huduma kupatikana katika Ofisi za Watendaji Kata na Vituo vya Tiba Vinavyotoa Huduma ya mama na Mtoto . Wageni hao watatembelea Vituo vya Usajili katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya na pia katika Ofisi kuu za NIDA zilizopo Kibaha Mkoani Pwani.

Album Pictures