Swahili   |   English
Usajili wa Vifo

Kifo hutakiwa kusajiliwa ndani ya siku 30, hata hivyo sheria inaruhusu usajili uliochelewa. Jukumu la kusajili wa vifo liko katika wafuatao:

  • Daktari aliyethibitisha kifo, au
  • Ndugu wa karibu wa marehemu ambao walikuwepo wakati wa kifo chake au walikuwepo wakati wa mwisho wa ugonjwa wake, au
  • Mmiliki wa nyumba, au mkazi wa nyumba, au mtu yeyote aliyechukua jukumu la kumzika marehemu huyo.
Huduma hizi zinapatikana kidigitali  bofya menu ya eRITA kupata huduma hizo:-

1: Usajili wa kifo ndani ya siku 30

    Iwapo kifo kimetokea hospitalini, kwenye kituo cha afya au katika zahanati, hakikisha unapata Kibali cha Mazishi. Ikitokea kifo kimetokea nyumbani toa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji, au kwa Msajili wa Wilaya kupata kibali cha mazishi. Jambo hili lifanyike ndani ya siku 30.
  • Wasilisha kibali cha mazishi kwa Msajili wa wilaya ambaye kifo kimetokea katika eneo lake la utendaji.
  • Lipa ada inayotakiwa kupata cheti (ada ya sasa ni Tsh. 7,000/=).


2: Usajili wa kifo uliochelewa

  • Jaza taarifa kifo katika mfumo wa kidigitali kisha ambatisha nyaraka za kuthibitisha (kumbukumbu za kikao cha familia na Barua kutoka kwenye mamlaka za serikali zinazohusika mfano Kata, Ofisa Mtendaji, Ofisa Mtendaji wa Kijiji) kuthibitisha kifo hicho.
  • Wasilishakitambulisho cha mwombaji
  • Barua ya utambulisho wa Mwombaji kutoka kwa Mtendaji Kata.
  • Lipa ada inayotakiwa  iwapo kifo kina zaidi ya siku 30 na chini ya miaka 10 ada ya sasa ni Tsh. 8,000/=
  • Lipa ada inayotakiwa  iwapo kifo kina zaidi ya miaka 10 ada ni Tsh. 20,000/=.


3: Uthibitisho wa Vyeti vya vifo

  • Wasilisha nakala ya cheti husika.
  • Lipa ada inayotakiwa (ada ya sasa ni Tsh. 6000/=).


4: Usajili wa Kifo kilichotokea nje ya nnchi 

  • Wasilisha nakala ya cheti cha kifo kutoka nnchi kifo kilipotokea.
  • Pasi ya kusafiria ya marehemu
  • Taarifa /cheti cha matibabu
  • Barua kutoka Ubalozi wa Tanzania  wa nnchi kifo kilipotokea ya kutaarifu RITA kifo hicho.
  • Kitambulisho cha Mtoa taarifa
  • Lipa ada inayotakiwa (ada ya sasa ni Tsh. 30,000/=).

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti

  • Wasilisha maombi ya masahihisho.
  • Ambatisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako.
  • Wasilisha cheti kinachotakiwa kufanyiwa masahihisho.
  • Lipa ada inayotakiwa pale maombi yanapokubalika (ada ya sasa ni Tsh. 13,000/=).

>>> MASWALI MBALI MBALI YANAULIZWA KUHUSU VIFO