Swahili   |   English
Udhamini

HUDUMA ZA UDHAMINI KWA NJIA YA MTANDAO

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) unapenda kuufahamisha Umma kwamba sasa  wanaweza kupata huduma za Udhamini kwa njia ya Mtandao,Huduma hizo ni :- 

  1. Miunganisho ya Wadhamini 
  2. Kutaarifu juu ya mabadiliko ya jina la chombo/au marekebisho .
  3. Kutaarifu juu ya mabadiliko ya wadhamini.
  4. Marejesho ya Wadhamini.
  5. Taarifa ya kubadili anwani ya Posta.
  6. Taarifa ya kubadili Dhamana / katiba.
  7. Kupata kibali cha kumiliki ardhi
  8. Upekuzi wa Taarifa za Wadhamini.
  9. Kuthibitisha nakala ya Nyaraka.
  10. Kupata nakala ya nyaraka

Mambo muhimu ya kuzingatia katika huduma za Udhamini:

  1. Tunza taarifa ulizotumia kufungua akaunti,
  2. Mwombaji awe na taarifa zake sahihi za Udhamini
  3. Waombaji wawe na kitambulisho cha Utaifa/ Kadi ya mpiga kura/ Hati ya kusafiria (Travelling passport) na vibali vya makazi kwa wageni.
  4. Kuwa na  cheti cha usajili kutoka mamlaka husika kwa asasi ambazo zimesajili katika mamlaka nyingine
  5. Mwombaji atapata Ankara ya malipo na atatakiwa kulipa kwa njia ya Benki (NMB and CRDB) au Mitandao ya simu (M-PESA, TIGO PESA and AIRTEL Money) .
  6. Mwombaji awe na nakala laini (soft copies) za viambatanisho vinavyotakiwa katika mfumo wa pdf,

Aidha, Tunapenda kuwasisitizia waombaji wote kufuata maelekezo hapo juu ili kuepuka usumbufu.

Anuani ya maombi ya Huduma ya Udhamini  pamoja na Mwongozo wa maombi ya huduma yanapatikana hapo chini ya ukurasa huu

Kumbuka: maombi hayatafanyiwa kazi kabla ya kukamilisha malipo ya ada ya huduma husika.Pia lazima kila asasi ijisajili kupata huduma zingine za udhamini.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0800 117 482