TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA Taratibu za kuandika wosia zinatofautiana kulingana na sheria ya mirathi inayotumika.
1. WOSIA WA MAANDISHI
Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika. Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia na mwingine ambaye sio ndugu wa karibu.Wosia na unatakiwa uwe na tarehe, uandikwe kwa karamu ya wino au upigwe chapa na uwe na saini ya mtoa wosia na saini za mashuhuda ambapo wote wanatakiwa kutia saini zao kwa wakati mmoja.
Mtoa wosia asiye jua kusoma ua kuandika awe na mashuhuda wa nne wanao jua kusoma na kuandika,muhusia huyo aweke alama ya kidole gumba cha mkono wake wa kulia,mashuhuda hao wote washuhudie na waweke saini zao kwenye Wosia kwa wakati mmoja.
2. WOSIA WA MDOMO/MATAMSHI
Wosia huu unashuhudiwa na mashuhuda wasiopungua wa nne wawili kati yao ndugu wa mtoa wosia na wawili waliobaki wasio ndugu wa mtoa wosia.Wosia huu utolewa na mtu asiye jua kusoma na kuandika.
TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA KATIKA SHERIA ZA MIRATHI
Wosia katika Sheria za kimila,zipo katika jedwali la 3 la Sheria ya (The Local Customary Law (Declaration|) No. 4 Order,1963.
Wosia katika Sheria za kiserikali,zipo katika sheria iliyorithiwa kutoka kwa Waingereza ya(The Indian Succession Act ),iliyopitishwa huko India mwaka 1865.
Hauna tofauti kubwa na wosia wa kimila isipokuwa wosia huu unatakiwa uwe katika maandishi.Vipengele vyote vya wosia wa maandishi vinatumika.
Mtoa wosia anaweza kufuta au kuongeza maneno mengine kwa kuandika maandishi mengine ambayo yatatakiwa kuzingatia masharti ya uandikaji wosia.
Wosia katika Sheria za kiislamu, mtoa wosia anaruhusiwa kuuusia 1/3 ya mali yake 2/3 lazima irithiwe na warithi halali.
UMUHIMU WA KUANDIKA WOSIA
Unaweka mambo bayana kuondoa utata kwa familia na jamaa zako.
Unamchagua msimamizi wa mirathi unayemtaka wewe.
Unatoa maelezo ya wapi mwili wako uhifadhiwe, taratibu zitakazotumika kuuzika mwili wako na jinsi gani mali yako igawanywe kama upendavyo wewe na kwa mujibu wa Sheria.
MASHARTI YA WOSIA
Mtoa wosia lazima awe na akili timamu.
Awe ametimiza miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
Uonyeshe tarehe,mwezi na mwaka ulioandikwa.
Uonyeshe majina ya warithi.
Mtoa wosia ahusishe mali zake binafsi na si za mtu mwingine.
Wosia ni siri wanufaika hawatakiwi kuujua.
Ushuhudiwe na mashaidi wawili, kwa mtoa wosia anaye jua kusoma na kuandika na kwa yule asiye jua kusoma ua kuandika mashuhuda wake lazima wawe wanne na wajue kusoma na kuandika.
Mtoa wosia lazima aweke saini yake,na kama hajui kusoma na kuandiaka aweke alama ya dole gumba la mkono wa kulia.
Mashuhuda lazima waweke saini zao tena kwa wakati mmoja.
SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA MTOA WOSIA KUTOMRITHISHA MRITHI WAKE
Kumtelekeza mtoa wosia pale ambapo anaumwa na kuhitaji msaada.
Kufanya uzinzi na mke wa mtoa wosia.
Endapo kifo cha mtoa wosia kitakuwa kimesababishwa na mrithi.