Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Usajili wa Ndoa

USAJILI WA NDOA NA TALAKA

RITA husajili Ndoa na Talaka, na pia hutoa vyeti. Usajili wa Ndoa na Talaka unaongozwa na Sheria ya Ndoa ya 1971 Sura ya 29 toleo la 2002.

 • Kupata nakala ya shahada ya Ndoa kutoka kwa Msajili wa Ndoa  Tanzania Bara.
 • Kupata nakala ya shahada ya Ndoa kutoka katika daftari la ndoa zilizofungwa nje ya nchi. 

 

 1. 1.    Kusajili ndoa inayodumu iliyokuwa haijasajiliwa

Mahitaji/Taratibu:

 • Jaza fomu zinazohusika (RGM 18RGMF 7).
 • Hati ya kiapo cha Ndoa (Ionyeshe kuwa Ndoa inadumu na haijasajiliwa).
 • Ambatisha nakala za vyeti vya uzazi wa watoto wa ndoa kama wapo.
 • Lipa ada halisi (ada ya sasa ni Tsh. 20000/=.

 

 1. 2.    Kupata cheti cha kutokuwa na kizuizi cha ndoa

Mahitaji/Taratibu

 • Jaza na wasilisha Fomu RGM 12.
 • Wasilisha nakala za cheti cha kuzaliwa na pasipoti.
 • Idhini ya maandishi ya mzazi/mlezi kuthibitisha kuwa mwombaji hana ndoa.
 • Kitambulisho cha mzazi au mlezi aliyeidhinisha kuwa mwombaji hana ndoa.
 • Lipa ada sahihi (ada ya sasa ni Tsh. 200,000/=).
 • Fomu inapaswa kuombwa na mwombaji.

 

Tanbihi: Iwapo muombaji anaishi ng'ambo, maombi yapitie Ubalozi wa Tanzania au Ubalozi mdogo katika nchi anayoishi.

 

 1. Kupata kibali cha kufunga ndoa ndani ya siku 7.

Mahitaji/Taratibu

 • Jaza Fomu RGMF. 9 
 • Thibitisha kimaandishi sababu za kutosha kwanini notisi ya siku 21 isitolewe.
 • Uwepo halisi wa wanandoa.
 • Wasilisha utambulisho wa wanandoa (pasipoti, kitambulisho cha kazi n.k)
 • Picha moja moja ya passport size
 • Kwa mgeni kutoka nje ya nchi anatakiwa awe na uthibitisho wa kutokuwa na ndoa toka nchini kwake au ubalozini.
 • Lipa ada halisi ambayo ni Tsh 100,000 kwa sasa ofisi za RITA

 

 1. 4.    Kibali cha kufunga ndoa mahali maalum

RITA (Msajili Mkuu) hutoa kibali maalumu cha kufunga ndoa mahali maalumu, zaidi ya mahali palipozoeleka kutumika kwa ibada au mikusanyiko.


Taratibu

 • Jaza Fomu RGM 4.
 • Toa sababu kwanini unataka kufunga ndoa katika sehemu ile na si mahali palipozoeleka.
 • Fomu hiyo isainiwe na kugongwa muhuri na mfungishaji ndoa (Katibu Tawala wa Wilaya au Kiongozi wa dini)
 • Lipa ada inayohusika (kwa sasa Tsh.200,000/=).
 • Ada kwa mgonjwa  ni  Tsh 20,000/=

 

 1. Maombi ya leseni ya kufungisha ndoa

Taratibu

 • Mkuu wa Taasisi ya Dini husika anapaswa kujaza form ya RGMF 2  (Endapo utajiombea mwenyewe, itakulazimu maombi yako yapitie kwa Mkuu wa Wilaya yako, ambaye atatoa maoni kuhusu ombi lako).
 •  Mwombaji ambaye ni mara yake ya kwanza atatakiwa aambatishe barua ya utambulisho toka kwa kiongozi wake, cheti cha usajili wa taasisi na picha mbili aina ya passport size.
 • Kama ni maombi ya kuhuisha leseni, ambatisha leseni yako ambayo muda wake umeisha pamoja na picha yako moja ya passport size.
 • Lipa ada ya maombi ya Tsh 30,000/=

 

>>> MASWALI MBALI MBALI YAYOULIZWA NA MAJIBU YAKE

 1. 1.    Ninawezaje kupata nakala ya cheti cha ndoa iwapo cheti halisi kilipotea?

Ndoa zote zinazofanyika Tanzania bara husajiliwa na kupata usajili wa msajili mkuu wa ndoa na talaka.  Wasajili wote wa wilaya na viongozi wa dini wanatakiwa kisheria kutuma ndoa zote walizozifungisha kila mwishoni mwa mwezi.  Kupitia katika taarifa hizi msajili mkuu kutunza kumbukumbu zote za ndoa.

 

Iwapo cheti halisi kimepotea unaweza kupata nakala ya usajili ya ingizo la ndoa ambalo  huhifadhiwa na msajili mkuu. 

Jinsi ya Kufanya ;

 • Wasilisha maombi yako kwenye ofisi za RITA ukionyesha majina ya wanandoa, mahali ilipofungwa, wilaya pia  onyesha iwapo ni ndoa ya kiserikali au ya kidini.
 • Lipa ada halisi ambayo kwa sasa ni Tsh. 50,000/= inayojumuisha yafuatayo: 
  - TSH 30,000/= ada ya utafutaji.
  - TSH 20,000/= ada ya cheti.
 1. Mimi ni Mtanzania ninayeishi ng’ambo na ninataka kuoa/kuolewa kulekule lakini mamlaka zinanitaka kuwapatia cheti kutoka Tanzania ambacho hakuna kipingamizi cha ndoa. Ninawezaje kukipata?
 • Nenda kwenye ubalozi wa Tanzania katika nchi unayoishi kupata fomu halisi ya maombi (kwa RGM 12) ambayo utapaswa kuijaza na kuiwasilisha kwa msajili mkuu wa ndoa kupitia katika ubalozi au (unaweza kupakua fomu hii kutoka kwenye tovuti yetu) au iwasilishe katika ofisi za RITA nchini Tanzania ikitokea upo hapa.
 • Maombi haya lazima yaambatane na nyaraka muhimu zinazoweza kukutambulisha kirahisi.  Nyaraka hizo zinajumuisha nakala ya pasipoti, cheti cha kuzaliwa, barua ya mzazi au mlezi kuthibitisha kwamba mwombaji hana ndoa na kitambulisho cha mzazi au mlezi aliyethibitisha.
 • Lipa ada ambayo kwa sasa ni Tsh. 200,000/=. 

  Tanbihi:
  Iwapo cheti hiki kitapaswa kutumwa kwako hakikisha kuwa malipo yanajumuisha gharama zozote za posta.
 1. 3.    Mimi ni Mtanzania ninayeishi ng’ambo. Nilifunga ndoa kule. Ninaweza kuisajili ndoa hii Tanzania?

Ndiyo:

Unaweza kuisajili ndoa hii kwa kuomba kwa msajili mkuu (ofisi za RITA) kwa kufanya yafuatayo:-

 • Jaza fomu ya RGMF 7 na RGM 11
 • Ambatisha nakala ya cheti chake cha ndoa aliyofunga nje ya nchi kilichothibitishwa na ubalozi na nakala ya tafsiri ya cheti cha ndoa kilichotafsiriwa na ofisa anayehusika au mthibitishaji wa umma kwa Kiingereza iwapo cheti kipo katika lugha nyingine tofauti na lugha ya kiingereza au Kiswahili kilichotafsiriwa na ofisa anayehusika au mthibitishaji wa umma .
 • Lipa ada inayotakiwa, kwa sasa ni Tsh. 100,000/=. 

  TANBIHI: 
  Ndoa iliyofungwa katika balozi za Tanzania za ng’ambo zinachukuliwa kama ndoa zilizofungwa Tanzania bara ambazo hazikufuata utaratibu huu.
 1. Kuna ndoa inayopaswa kusajiliwa na ninaona kuwa kuna vipingamizi kwenye ndoa hiyo, ninaweza kuviepuka?
 • Toa taarifa za vikwazo vyako kwa kuandika kwa msajili ambaye alipewa taarifa za mambo hayo.
 • Andika taarifa za vikwazo vyako kwa msajili mkuu wa ndoa na talaka
 • Iwapo unafikiri kuwa wana ndoa wanaweza kuamua kutoa taarifa mpya kwa msajili mwingine, andika vikwazo hivyo kwa msajili huyo.
 1. 5.    Ndoa nyingi zilivunjwa na mahakama. Ninawezaje kupata cheti cha talaka yangu?
 •  Wasilisha nakala ya cheti chako cha ndoa kwa msajili mkuu (RITA).
 • Wasilisha hukumu ya uvunjaji wa ndoa  na hati ya talaka ya mahakama.
 • Lipa ada ya lazima ambayo kwa sasa ni Tsh. 20000/=

  TANBIHI:
  Talaka yako itatambuliwa na kusajiliwa  iwapo muda uliowekwa kwa rufaa utakuwa umekwisha na hakukuwa na rufaa iliyokubaliwa na iwapo ilikubaliwa ilikwishasikilizwa na hakuna rufaa zaidi.
 1. 6.    Inawezekana kwa mtu kuchukua leseni ya kufungisha ndoa kwa niaba ya mtu mwingine?

Ndiyo: 

 • Kinachotakiwa ni kuleta kitambulisho chako, nakala halisi ya kibali kilichokwisha na barua ya utambulisho kutoka kwa mwombaji.
 1. 7.    Kwa ndoa iliyofungwa mwaka 1958 kabla ya Sheria ya ndoa ya 1971 haijaanza na ndoa yangu haikusajiliwa kwa sheria ya zamani (Sheria ya ndoa) lakini ndoa yangu bado inadumu. Ninaweza kuisajili ndoa hii na kupata cheti cha ndoa?
 • Omba kwa msajili mkuu wa ndoa (RITA) kwa kujaza fomu za RGMF . 7 na RGM 18.
 • Ambatisha ushahidi kwenye maombi haya kuthibitisha ndoa yako mfano cheti kilichotolewa na kiongozi wa dini au kadhi.
 • Ambatisha hati ya kiapo kuthibitisha kuwa ndoa hiyo bado inadumu.
 • Lipa ada muhimu ambayo kwa sasa ni Tsh. 20000/