RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
MEDIA CENTRE
March
10
2026
KIKAO CHA 34 CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI
News & Update
`

Kikao cha 34 cha Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kimefanyika Machi 10, 2026 Jijini Dodoma, ambapo kimewaleta pamoja viongozi na wawakilishi wa wafanyakazi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Wakala na ustawi wa watumishi.


Akizungumza katika kikao hicho maalum kwaajili ya kujadili mambo mbalimbali hususani bajeti ya Wakala kwa mwaka 2025/2026, Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi alielezea utekelezaji wa majukumu ya Wakala pia kujadili mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku. 

Aidha, kikao kilitoa nafasi kwa wajumbe kujadili na kuridhia maboresho ya bajeti ya wakala na kutoa mapendekezo yenye lengo la kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Baraza la Wafanyakazi linaendelea kuwa jukwaa muhimu la ushirikishwaji wa watumishi katika masuala ya maendeleo ya Wakala, hatua inayosaidia kuimarisha mshikamano, uwajibikaji na utendaji bora ndani ya RITA.