RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
June
16
2025
UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOA WA DAR ES SALAAM
News & Update
`
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wananchi kutumia fursa ya  Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) kupata huduma za msaada wa kisheria na mawakili bure ili kutatua changamoto za masuala ya kisheria.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Juni 16, 2025  Mhe. Majaliwa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata msaada wa kisheria huku akiwasisitiza wananchi kuandika Wosia ili kuepusha migogoro ya Kifamilia na kupunguza mashauri ya mirathi.

Aidha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amewaomba wananchi kufika katika maeneo yote yatakayofikiwa kupata msaada wa kisheria bure kwani fursa hiyo inawalenga wale wote wenye changamoto za maswala ya kisheria na wale wasio na uwezo wa kuwaajiri mawakili kwaajili ya kuwatetea