RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
MEDIA CENTRE
June
16
2025
UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOA WA DAR ES SALAAM
News & Update
`
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wananchi kutumia fursa ya  Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) kupata huduma za msaada wa kisheria bure pamoja na mawakili  ili kutatua changamoto za masuala ya kisheria.

Hayo ameyasema katika uzinduzi wa kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia leo Juni 16, 2025 Jijini Dar es Salaam huku akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata msaada wa kisheria huku akiwasisitiza wananchi kuandika Wosia ili kuepusha migogoro ya Kifamilia na kupunguza mashauri ya mirathi.

Aidha kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amewaomba wananchi kufika katika maeneo yote yatakayofikiwa kupata msaada wa kisheria bure kwani fursa hiyo inawalenga wale wote wenye changamoto za maswala ya kisheria na wale wasio na uwezo wa kuwaajiri mawakili kwaajili ya kuwatetea.