Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) unapenda kuwaalika Wajumbe wa Bodi za Wadhamini wa Taasisi za kidini, vyama vya siasa, vyama vya michezo na asasi za kiraia zilizopo katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Morogoro, Singida na Manyara katika mkutano utakaofanyika siku ya Alhamisi, tarehe 27 Novemba, 2025 katika Hoteli ya Saint Gasper jijini Dodoma kuanzia saa 2. 00 asubuhi. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Dkt. Juma Zuberi Homera(Mb).
Lengo la mkutano huo ni kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi za wadhamini ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Bodi za Wadhamini sura ya 318 pamoja na katiba za taasisi wanazozisimamia.
Aidha, wadhamini watapata nafasi ya kubadilishana uzoefu na kupata ufafanuzi wa masuala yanayohitaji miongozo ya kitaalam ikiwa ni pamoja na matumizi ya mfumo wa kidijitali wa eRITA.
Washiriki wote wanatakiwa kujisajili kupitia kiunganishi (link) kinachopatikana katika tovuti ya wakala www.rita.go.tz au kwa kupiga simu namba 0699 082 400.
Pamoja na mafunzo hayo, RITA itaendesha Kliniki maalumu kwa ajili ya kutoa huduma zote zinazohusiana na bodi za wadhamini pamoja na kutatua changamoto. Kliniki zitafanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na Morogoro kuanzia tarehe 01- 05 Disemba, 2025 saa 02:00 asubuhi.
Tags : #RITA