Bodi ya Ushauri ya Wizara (MAB)

Majukumu ya Bodi ya ushauri ya Wizara (MAB)

Bodi ya Ushauri ya Wizara itaundwa kumsaidia Waziri kuwa na mkakati wa uendeshaji.Mwenyekiti wa Bodi atakuwa Katibu Mkuu na litakuwa na wajumbe wachache wa wadau wakuu wanaohusika, ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa wateja wa Wakala.


Bodi ya Ushauri ya Wizara itatoa ushauri kwa waziri juu ya yafuatayo:

  • Maendeleo na urekebishaji wa muundo wa sera.
  • Malengo ya RITA.
  • Ukubalifu wa mkakati na mpango wa shughuli na bajeti zinazohusika za Kabidhi Wasii Mkuu.
  • Uwekaji wa vipaumbele na malengo ya utendaji kwa mwaka wa Wakala.
  • Ukubalifu wa ripoti za Mwaka na Taarifa za fedha.
  • Tathmini ya Utendaji wa Baraza.
  • Na suala lingine lolote lililomo kwenye Sheria ya Wakala Na. 30 ya 1997.
  • Masuala mengine yoyote zaidi yanayolihusu RITA pale Waziri atakapoona umuhimu kwa nyakati mbalimbali yataelekezwa kwenye Bodi.

WAWAKILISHI WA BODI YA RITA (NANI NI NANI KATIKA BODI)

  1. Bw. Vicent F. Mrisho   -           Mwenyekiti
  2. Bw. Phillip G. saliboko  -         Katibu
  3. Bw. August B. Kowero  -          Mjumbe
  4. Bi. Suzan B. Mkapa        -      Mjumbe
  5. Bw. John J. Kyaruzi       -        Mjumbe
  6. Bw. Magnus Ulungi     -          Mjumbe
  7. Bi. Salome S. Mollel      -        Mjumbe – Mwakilishi wa Wizara Mama
Rita Internal Search

Matangazo
Video / Picha
Sheria



Events Calendar
September 2010
SunMonTueWedThuFriSat
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930