Miunganisho ya Wadhamini unaviwezesha vyombo visivyoshirikishwa kuwa na uwezo binafsi wa kisheria wa kufungulia na kufunguliwa shitaka katika jina la asasi, kumiliki mali na kuachia mali.
Taratibu / Mahitaji:
- Wasilisha Fomu ya Maombi TI.1 na kiambatanishi "A" ikiambatishwa na Waraka wa Katiba ya asasi unaoomba kushirikishwa (Nakala 3).
- Wasilisha picha ndogo 3 za wadhamini waliopendekezwa, na wasifa wao.
- Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambayo chombo hicho kina makao yake makuu.
- Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika sekta ya Serikali ambapo asasi inayotaka kuunganisha wadhamini wake inaangukia (kama ni asasi isiyo ya kidini).
- Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika asasi kuu za kidini iwapo kinachoomba ni asasi ya kidini.
- Lipa ada halisi/ada ya sasa ni Tsh. 100,000/=.
Tanbihi:
1: Msimamizi Mkuu wa Wadhamini halazimika kuunganisha muunganisho wa Wadhamini pindi mahitaji ya hapo juu yasipotekelezwa.
2: Kutaarifu juu ya mabadiliko ya jina la chombo.
- Nyaraka zote zinazowasilishwa ziwe Nakala mbilimbili isipokuwa Barua ya Mapendekezo.
- Mara baada ya kuunganishwa, muunganisho huu unakuwa na wajibu ufuatao:
- Hairuhusiwi kumiliki ardhi au haki kwenye ardhi, bila kupata kibali cha maandishi kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa wadhamini (Kabidhi Wasii Mkuu).
- Kumtaarifu Msimamizi Mkuu wa wadhamini juu ya mabadiliko yoyote, mabadiliko ya wadhamini, jina la chombo, anwani ya posta, Katiba ndani ya mwezi mmoja.
- Kuwasilisha marejesho ya wadhamini kujaza fomu T.1.5 kila baada ya muda wa miezi kumi na miwili .
Taratibu / Mahitaji3: Kutaarifu juu ya mabadiliko ya wadhamini.
- Jaza na wasilisha Fomu ya TI.2 na TI.3.
- Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu ya mkutano uliothibitishwa ambao ulifanya mabadiliko ya jina.
- Rejesha cheti halisi cha zamani .
- Lipa ada halisi Fomu za TI. 2 na TI. 3 Tsh 20,000/= kila moja, cheti 5,000/=
Taratibu / Mahitaji4: Marejesho ya Wadhamini.
- Jaza na wasilisha Fomu ya TI. 4
- Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu za kikao rasmi ambacho kilifanya mabadiliko ya Wadhamini.
- Lipa ada halisi ya Tsh. 20,000/=.
Taratibu / Mahitaji5: Taarifa ya kubadili anwani ya Posta.
- Jaza na wasilisha Fomu ya TI.5
- Lipa ada halisi ya Tsh. 10,000/=.
Taratibu / Mahitaji6:Taarifa ya kubadili Dhamana / katiba.
- Jaza na wasilisha Fomu ya TI.6
- Lipa ada halisi ya Tsh. 20,000/=.
Taratibu / Mahitaji7.Kupata kibali cha kumiliki ardhi.
- Jaza na wasilisha Fomu ya TI. 7
- Lipa ada halisi (ada ya sasa ni Tsh. 20,000/=).
- Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu za kikao rasmi kilichoamua mabadiliko ya dhamana / katiba.
Taratibu / Mahitaji8.Upekuzi wa rekodi za Wadhamini.
- Wasilisha barua ya maombi ukielezea matumizi yanayokusudiwa ya ardhi .
- Wasilisha nakala iliyodhibitishwa ya barua ya toleo/mkataba wa uuzaji/waraka wa ubadilishaji mmiliki.
- Lipa ada halisi ya Tsh. 20,000/=.
Taratibu / Mahitaji9.Kupata nakala iliyothibitishwa.
- Wasilisha maombi ya upekuzi.
- Lipa ada halisi ya Tsh. 5,000/=
Taratibu / Mahitaji
- Wasilisha maombi .
- Lipa ada halisi ya Tsh. 3,000/= kwa nakala iliyoombwa.
- Lipa ada ya Tsh. 3,000/= kwa uthibitisho wa ofisi

