Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) unapenda kuufahamisha Umma kwamba sasa unaweza kutuma maombi ya kupata huduma zifuatazo kwa njia ya Kidigitali:
HUDUMA ZA VIZAZI NA VIFO
Huduma zinazopatikana kidigitali:
- 1. Cheti cha Kuzaliwa
- 2. Cheti cha kuzaliwa cha zamani kwenda kipya
- 3. Uhakiki wa cheti cha Kuzaliwa
- 4. Cheti cha Kifo
- 5. Cheti cha kifo cha zamani kwenda kipya
- 6. Uhakiki wa cheti cha Kifo
Bofya hapa kupata huduma
HUDUMA ZA NDOA NA TALAKA
Huduma zinazopatikana kidigitali:
- 1. Maombi ya leseni ya kufungisha ndoa
- 2. Maombi ya Shahada ya kufungisha ndoa
- 3. Kupata kibali cha kufunga ndoa ndani ya siku 7
- 4. Kupata cheti cha kutokuwa na kipingamizi cha ndoa
- 5. Kusajili ndoa inayodumu iliyokuwa haijasajiliwa
- 6. Kibali cha kufunga ndoa mahali maalum
- 7. Kusajili Ndoa
- 8. Kusajili ndoa iliyofungwa nje ya nchi
- 9. Kusajili Talaka
- 10. Kusajili Talaka iliyotolewa nje ya nchi
Bofya hapa kupata huduma
HUDUMA ZA BODI ZA WADHAMINI
Huduma zinazopatikana kidigitali:
- 1. Miunganisho ya Wadhamini
- 2. Kutaarifu juu ya mabadiliko ya jina la chombo
- 3. Marejesho ya wadhamini
- 4. Taarifa za kubadili anuani
- 5. Kupata kibali cha kumiliki ardhi
- 6. Upekuzi wa taarifa za wadhamini
- 7. Kuthibitisha nakala za nyaraka
- 8. Kupata nakala za nyaraka
Bofya hapa kupata huduma