Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Mkakati wa Usajili wa Watoto chini ya miaka Mitano

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini utazindua mpango mkakati wa Usajili wa Kisasa wa Watoto Chini ya miaka mitano. Mpango  unalenga kuongeza idadi kwa kiasi kikubwa cha Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano, sambamba na kuboresha mfumo wa usajili Tanzania Bara. Mpango huu ni kuweka upya /pamoja mfumo wa  Usajili. Maana kazi ya usajili zitahama kutoka serikali kuu kwenda ofisi za serikali za mitaa. Utekelezaji wa mfumo huu utafanyika kwa mifumo ya afya na serikali za mitaa iliyopo.

Kulingana na mkakati, vyeti vya kuzaliwa vya kuandikwa na mkono vitatolewa bure kwa watoto chini ya miaka mitano na huduma hii inapatikana katika  ofisi za Afisa Mtendaji wa Kata na ofisi za (MCH) Afya ya mama na mtoto. Kama mzazi atahitaji nakala ya cheti cha mtoto cha Kompyuta, huduma hiyo itakuwa inapatikana kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (Mkurugenzi)na huduma hiyo italipiwa.

Mpango Mkakati huu wa usajili umezinduliwa katika mkoa wa Mbeya ,mpango huu ni endelevu na  utatekelezwa katika Halmashauri zote katika mkoa wa Mbeya. Na baadae Maradi huu utakwenda katika Mikoa Mingine Tanzania Bara.

Mpango huu umeshatekelezwa katika Miko kumi na mmoja (11) ambayo ni Mbeya ,Songwe,Mwanza,Iringa,Njombe,Shinyanga,Geita, Lindi,Mtwara,Mara na Simiyu.

NB:Kwa Mikoa ambayo ipo ndani ya  mradi wa U5 na mtoto yuko chini ya miaka mitano cheti ni bure ila kama amepoteza au kuharibika itampasa mzazi au mlezi kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri anakoishi  atalipia shs.5000/= na kupatiwa cheti kingine kwa taarifa zilezile za awali.