Swahili   |   English
Lengo na Usuli wa Historia

Lengo
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) inakusudia katika utoaji wa habari nzuri na thabiti juu ya matukio muhimu maishani, uunganishaji wadhamini, utunzaji wa mali chini ya udhamini, za mtu aliyefariki, muflisi, na watoto walio chini ya umri wa utu uzima ili kuwezesha sheria kuchukua mkondo wake.

Usuli wa kihistoria
RITA ilizinduliwa rasmi tarehe 23 Juni 2006 na inachukua nafasi ya ile iliyoitwa Idara ya kabidhi Wasii Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, Wizara ya Katiba na Sheria. Ni Wakala chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika Wizara ya Katiba na Sheria.

Historia ya RITA inaanzia nyuma mnamo mwaka 1917 wakati serikali ya kikoloni ya Ujerumani ilipotunga sheria ya usajili wa vizazi na vifo (Tangazo Na. 15 ya 1917 (Eneo la wananchi). Wakati Waingereza walipoichukua Tanganyika (Tanzania Bara) kutoka kwa Wajerumani waliutambua utaratibu wa usajili wa vizazi na vifo uliowekwa kwa sheria za Kijerumani kwa kutambua daftari chini ya Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, 1920 (sura ya 108).
Ikumbukwe kwamba chini ya mataifa yote mawili ya kikoloni usajili wa vizazi na vifo haukuwa wa lazima kwa Waafrika.

Kati ya mwaka 1920 na 1960 serikali ya kikoloni ya Kiingereza ilikuja na sheria zaidi kuhusu matukio muhimu ya kimaisha na masuala mengine. Sheria hizi ama zilisimamiwa kwa ujumla au kwa sehemu yake na ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu/Msajili Mkuu. Sheria hizi ni:- 

Wakati Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961 Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba ilianzishwa. Miongoni mwa Idara za Wizara ilikuwa Idara ya Msajili Mkuu na Idara ya Mtawala Mkuu. Kila moja ya idara hizi ilikuwa na Sheria zake za kuzisimamia:

(a) Ofisi ya Msajili Mkuu

 

(b) Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu

Kufuatia mabadiliko kadhaa ya Sera ya serikali baada ya Azimio la Arusha na kutambuliwa kwa Wizara mbalimbali mnamo 1967, wizara ya Sheria ilivunjwa na Idara mbalimbali, zilizokuwa ndani ya wizara hiyo, zilihamishiwa kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kama Divisheni ambayo ilijulikana kama Divisheni ya Sheria. Idara mbili za Kabidhi Wasii Mkuu na Msajili Mkuu ziliunganishwa kuwa idara moja iliyojulikana kama idara ya Kabidhi Wasii Mkuu. Baadhi ya sheria zilizokuwa zinasimamiwa na ofisi ya Msajili Mkuu zilipelekwa katika:


1. Msajili wa Vyama vya Hiari(Wizara ya Mambo ya Ndani).

2. Msajili wa makampuni (Wizara ya Biashara na Viwanda).

3. Msajili wa Miliki (Wizara ya Ardhi na Makazi).

Idara ya Kabidhi Wasii Mkuu ilipewa majukumu yanayoonyeshwa katika sheria ambayo yameorodheshwa hapa chini:

RITA imeundwa kuchukua majukumu ambayo yalikuwa yakifanywa na Idara ya Kabidhi Wasii Mkuu. Majukumu hayo yapo kwenye Sheria zifuatazo:

Wakala una wafanyakazi 132. RITA makao makuu wafanyakazi 93 na kwenye ofisi za wilayani wafanyakazi 39. Wakala una ofisi zake wilayani, lakini zaidi hutegemea na kushirikiana na mamlaka za wilaya na mikoa ili kuendesha shughuli zake vizuri.

Wakala unahodhi shughuli za usajili wa vizazi, vifo, ndoa talaka na miungano ya wadhamini. Kutokana na uchumi huria shughuli za wakala zinazohusu upokeaji na ufilisi wa Kampuni zinaelekea kuhuishwa kutoka katika kukwama wakati wa miaka ya kipindi cha Azimio la Arusha.