Swahili   |   English
Udhamini wa Umma
Urithi wa mrithi aliye chini ya umri

Msimamizi wa mirathi ikiwa ni pamoja na Kabidhi Wasii Mkuu baada ya kufikia hatua kurithisha mali kwa warithi, na endapo kuna mrithi aliye chini ya umri, na hakuna mtu yeyote aliye tayari kuwa mlezi, na kupokea hisa za mrithi huyu, basi msimamizi atakabidhi hisa za mrithi huyu kwa mdhamini wa umma. Mdhamini atashikilia hisa hizo hadi mtoto huyo atakapofikia umri wa utu uzima, ambapo atamkabidhi.

Mali itakayokosa mmiliki


Mahakama kuu baada ya kuombwa na mwanasheria Mkuu inaweza kuteua Wadhamini wa Umma kuwa mdhamini wa mali yenye asili ya umma ikiwa imethibitishwa na mahakama kuridhika kuwa hakuna mtu Tanzania bara anayependa na mwenye uwezo wa kushikilia mali hiyo hadi maagizo zaidi ya mahakama au mtu aliyepangwa atakapojitokeza.

Taratibu / mahitaji
  • Mtu mwenye uchungu na mali husika, atamuarifu Mwanasheria Mkuu juu ya kuwepo na mali ya umma isiyo na mmiliki, au inayoelekea kukosa mmiliki .
  • Mwanasheria Mkuu atapeleka maombi Mahakama Kuu chini ya Sheria ya Mdhamini wa Umma Sura ya 31 toleo la 2002.
  • Mdhamini wa Umma atateuliwa kusimamia mali hadi maagizo zaidi ya mahakama au mtu aliyepangwa atakapojitokeza.