Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Bodi ya Ushauri ya Wakala (MAB)

Majukumu ya Bodi ya ushauri ya Wakala (MAB)

Bodi ya Ushauri ya Wakala ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili  ya kumshauri Afisa Mtendaji Mkuu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wakala.


Bodi ya Ushauri ya Wakala itatoa ushauri kwa Afisa Mtendaji Mkuu juu ya yafuatayo:

  • Maendeleo na urekebishaji wa muundo wa sera.
  • Malengo ya RITA.
  • Ukubalifu wa mkakati na mpango wa shughuli na bajeti zinazohusika za Kabidhi Wasii Mkuu.
  • Uwekaji wa vipaumbele na malengo ya utendaji kwa mwaka wa Wakala.
  • Ukubalifu wa ripoti za Mwaka na Taarifa za fedha.
  • Tathmini ya Utendaji wa Baraza.
  • Na suala lingine lolote lililomo kwenye Sheria ya Wakala Na. 30 ya 1997.
  • Masuala mengine yoyote zaidi yanayolihusu RITA pale Afisa Mtendaji Mkuu atakapoona umuhimu kwa nyakati mbalimbali yataelekezwa kwenye Bodi.