Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Usajili wa Ndoa

RITA husajili Ndoa na Talaka, na pia hutoa vyeti. Ndoa na Talaka vinaongozwa na Sheria ya Ndoa ya 1971 Sura ya 29 toleo la 2002.

 • Kupata nakala ya shahada ya Ndoa kutoka kwa Msajili wa Ndoa katika Tanzania Bara.
 • Kupata nakala ya shahada ya Ndoa kutoka daftari la ndoa zilizofungwa nje ya nchi. 

Mahitaji/Taratibu:

 • Wasilisha nakala ya cheti cha Ndoa au maelezo juu ya Ndoa (majina ya wanandoa, tarehe ya ndoa na mahali palipofungiwa Ndoa)..
 • Wasilisha namba ya kuingizwa kwenye daftari la Ndoa.
 • Lipa ada halisi (ada ya sasa ni Tsh. 20000/=).


1. Kusajili ndoa inayodumu iliyokuwa haijasajiliwa.

Mahitaji/Taratibu:
 • Jaza fomu zinazohusika (RGM 18RGM 7).
 • Hati ya kiapo cha Ndoa (Ionyeshe kuwa Ndoa inadumu na haijasajiliwa).
 • Ambatisha nakala za vyeti vya uzazi wa watoto wa ndoa kama wapo.
 • Lipa ada halisi (ada ya sasa ni Tsh. 20000/=.
2. Kupata cheti cha kutokuwa na kizuizi cha Ndoa.
Mahitaji/Taratibu
 • Jaza na wasilisha Fomu RGM 12.
 • Wasilisha nakala za cheti cha kuzaliwa, pasipoti kama ipo.
 • Idhini ya maandishi ya mzazi/mlezi.
 • Lipa ada sahihi (ada ya sasa ni Tsh. 200,000/=).
 • Fomu inapaswa kuombwa na mwombaji.
Tanbihi: Iwapo muombaji anaishi ng'ambo, maombi yapitie Ubalozi wa Tanzania au Ubalozi mdogo katika nchi anayoishi.

3. Kupata kibali cha kusherehekea ndoa ndani ya siku 7.
Mahitaji/Taratibu
 • Jaza Fomu RGM 4.
 • Thibitisha kimaandishi sababu za kutosha kwanini notisi ya siku 21 isitolewe.
 • Uwepo halisi wa wanandoa.
 • Wasilisha utambulisho wa wanandoa (pasipoti, kitambulisho cha kazi n.k)
 • Lipa ada halisi kwa ofisi za RITA Wilaya (ada ya sasa Tsh. 33,000/= kwa ndoa ya kiserikali na 11,000/= kwa ndoa ya kidini).
 • Lipa ada halisi kwa RITA MAKAO MAKUU(ada ya sasa Tsh.38,000/= kwa ndoa ya kiserikali na 16,000).
 • 4. Kibali cha kufunga ndoa mahali maalumu.

   RITA (Msajili Mkuu) hutoa kibali maalumu cha kufunga ndoa mahali maalumu, zaidi ya mahali palipozoeleka kutumika kwa ibada au mikusanyiko.

Taratibu
 • Jaza Fomu RGMF 4.
 • Toa sababu kwanini unataka kufunga ndoa katika sehemu ile na si mahali palipozoeleka.
 • Lipa ada inayohusika (kwa sasa Tsh.100000/=).
5. Maombi ya kufungisha ndoa sehemu maalumu.
Taratibu.
 • Mwombe mkuu wako au uongozi wa shirika lako wajaze fomu RGM 2 (Endapo utajiombea mwenyewe, itakulazimu maombi yako yapitie kwa mkuu wa wilaya yako, ambaye atatoa maoni kuhusu ombo lako).
 • Kama ni maombi ya kuhuisha leseni, ambatanisha leseni yako ambayo muda wake unaisha.
 • Lipa ada ya maombi (kwa sasa Tsh.200000/=).

>>> MASWALI MBALI MBALI YAYOULIZWA