Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           MAFUNZO KWA VIONGOZI WA DINI

Description: RITA YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA DINI KUHUSU HUDUMA YA WOSIA, MIRATHI, NDOA, TALAKA PAMOJA NA UDHAMINI WILAYANI KOROGWE - TANGA. *Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umetoa semina ya siku moja kwa viongozi wa dini kwa ngazi ya wilaya, tarafa na kata kuhusu huduma za Wosia, Mirathi, Ndoa, Talaka pamoja na Udhamini. Kwa kutambua umuhimu mkubwa wa viongozi hao katika kukamilisha huduma hizo, Wakala ukaandaa mafunzo hayo ili kuzidi kuongeza uelewa kwa viongozi hao juu ya huduma hizo lakini pia kutambua changamoto wanazopitia katika utendajikazi wao na jinsi ya kuzikabili. *Mafunzo hayo ya siku moja yalihudhuriwa na viongozi kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya Korogwe, Bi. Kissa Kasongwa.

Album Pictures