Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           Ziara Namtumbo Ruvuma

Description: Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dr. Damas Ndumbaro ametembelea na Kukagua Utekelezaji wa Majukumu ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini( RITA) katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma. Katika ziara hiyo alipewa Ripoti ya hali ya Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka na pia kujionea kwa vitendo kazi inavyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Katika Kituo cha Tiba ambacho kinatoa huduma ya Usajili na kutoa vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano. Akiongea na Viongozi wa Wilaya Mhe. Ndumbaro amesema kwamba Serikali kupitia Wizara yake imedhamiria kuifanya RITA iendeshe shughuli zake kidigitali ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi hasa wa Vijijini kupata huduma kwa Urahisi

Album Pictures