Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainab Katimba, ametembelea na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayoendelea mkoani Dodoma.
Katika ziara hiyo, alipata fursa ya kufika katika banda la Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) na kuzungumza na wananchi pamoja na wataalamu wanaotoa huduma.
Aidha, Mhe. Katimba aliwapatia vyeti vya kuzaliwa wananchi waliofika kupata huduma hiyo inayotolewa na RITA katika kampeni hiyo ya msaada wa kisheria na pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kutumia kampeni hiyo kupata elimu na ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za kisheria.