Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, DKT. Anna Peter Makakala, ametembelea banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) katika Maonesho ya 50 ya Kitaifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) na kupata maelezo ya huduma za Wakala.
Katika ziara hiyo, Dkt. Makakala amepongeza maelezo ya kina kuhusu utendaji kazi wa Wakala, ambapo pia amepata fursa ya kutembelea maeneo matatu tofauti ndani ya banda hilo ili kushuhudia jinsi wananchi wanavyohudumiwa kwa ukaribu ma kutoa wito kwa RITA kuongeza nguvu katika kutoa elimu ya Amana ya Familia (Family Trust) ili iweze kuwafikia na kuwasaidia wananchi wengi zaidi nchini.
Katika maonesho hayo, RITA inaendelea kutoa huduma na elimu kwa umma katika maeneo mbalimbali ikiwemo Usajili wa Vizazi na Vifo, Ndoa na Talaka, Kuandika na kuhifadhi Wosia na Elimu ya amana ya familia (Family Trust)