RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
August
08
2026
NAIBU KABIDHI WASII MKUU BI. IRENE LESULIE AKIWAHUDUMIA WANANCHI WALIOTEMBELEA BANDA LA RITA KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE.
News & Update
`

Maonesho ya 33 ya Kitaifa ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea jijini Dodoma yamekuwa zaidi ya jukwaa la kilimo; yamekuwa sehemu muhimu inayowaunganisha wananchi na huduma za Serikali. Kila siku, mamia ya wananchi hutembelea mabanda mbalimbali kutafuta taarifa, kupata elimu na kutatuliwa changamoto zinazohusu huduma wanazozihitaji.

Katika ziara yake, Naibu Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA, Bi. Lesulie amezungumza na wananchi, amesikiliza changamoto zao na kuwapatia huduma pamoja na maelekezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na RITA. Hatua hiyo imeonyesha dhamira ya uongozi wa RITA ya kuwa karibu na wananchi na kuhakikisha kila anayefika anapata huduma bora, sahihi na kwa wakati.

Katika banda la Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za usajili wa matukio muhimu ya binadamu ikiwemo kupata vyeti vya kuzaliwa kwa wanaokamilisha taratibu husika. Wengi wameeleza kufurahishwa na urahisi wa huduma hizo.

Mbali na kutoa huduma, maafisa wa RITA wanaendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kusajili matukio muhimu kwa wakati na matumizi ya nyaraka sahihi za utambulisho katika kupata huduma mbalimbali.

Kwa wengi wanaotembelea banda la RITA, katika maonesho hayo imekuwa fursa ya kupata suluhisho, kujifunza na kuondoka wakiwa wamekamiliaha huduma walizozifuata kwa urahisi, haraka na kwa wakati.