Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini ametembelea banda la RITA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara (SABASABA) na kuongea na wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma ya usajili na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Pia, Mhe. Sagini alipata maelezo kutoka kwa Afisa Usajili Bi. Victoria Mushi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa katika kipindi chote cha maonesho hayo.
''kama unavyojionea mwenyewe Mhe. Waziri, kwa upande wetu tumejipanga vizuri na wananchi wanafurahia huduma zetu kwani wanatuma maombi yao kidijitali kupitia eRITA kisha tunawaandalia vyeti na kuwapatia hapa hapa sabasaba.'' Alisema Bi. Mushi