RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
MEDIA CENTRE
July
01
2026
MHE. ZAINAB KATIMBA ATEMBELEA BANDA LA RITA KUONA HUDUMA ZITOLEWAZO KATIKA MAONESHO YA 50 YA KIMATAIFA YA BIASHARA DAR ES SALAAM
News & Update
`

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba, ametembelea banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) katika Maonesho ya 50 ya Kitaifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) na kupongeza Wakala kwa utoaji wa huduma bora kwa jamii.

Katika ziara hiyo, Mhe. Katimba amepongeza  maelezo ya kina kuhusu utendaji kazi wa Wakala,  ambapo pia amepata fursa ya kutembelea maeneo matatu tofauti ndani ya banda hilo ili kushuhudia jinsi wananchi wanavyohudumiwa kwa ukaribu ma kutoa wito kwa RITA kuongeza nguvu katika kutoa elimu ya Amana ya Familia (Family Trust) ili iweze kuwafikia na kuwasaidia wananchi wengi zaidi nchini.

Katika maonesho hayo, RITA inaendelea kutoa huduma na elimu kwa umma katika maeneo mbalimbali ikiwemo Usajili wa Vizazi na Vifo, Ndoa na Talaka, Kuandika na kuhifadhi Wosia na Elimu ya amana ya familia (Family Trust)