RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
MEDIA CENTRE
July
20
2026
KAMPENI YA USAJILI WA VYETI YA KUZALIWA WILAYA YA TEMEKE YAENDELEA KATIKA KATA YA CHAMAZI.
News & Update
`

Wananchi wa Kata ya Chamazi na Mbande wameendelea kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa inayoendelea, huku wakiipongeza Serikali kupitia Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kusogeza huduma hiyo karibu na makazi yao.

Baadhi ya wananchi wamesema huduma hiyo imewaondolea usumbufu wa kusafiri umbali mrefu na imewapa fursa ya kupata vyeti vya kuzaliwa kwa urahisi. Pia wamewahimiza wananchi wengine kutumia fursa hiyo kabla kampeni haijafikia tamati.

Kampeni hiyo inaendelea katika Kata ya Chamazi na eneo la Mbande kuanzia tarehe 9 hadi 28 Julai 2026.