Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Mkakati wa Usajili wa Watoto walio na Umri kati ya Miaka 5-17

Mkakati wa Usajili wa Watoto walio na Umri kati ya Miaka 5-17

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umebuni programu ya Usajili na Kutoa vyeti katika Shule za Msingi katika Mikoa na wilaya mbalimbali Tanzania Bara.

kwa kuanza mikoa ya mwanzo kufikiwa na programu hii ni Igunga Mkoa wa Tabora, Dar es Salaam, Njombe,Tunduru na Musoma. Zoezi hili  ni sehemu ya utekelezazji wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio na Umri kati ya Miaka 5-17 ( 5-17 Birth Registration Initiative) uliobuniwa ili kukabiliana na changamoto ya wananchi wengi kutosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa.

RITA imeshirikiana na idara ya Elimu kuendesha mkakati huu katika kila Mkoa na Wilaya Husika kisha walimu waratibu hufanyiwa mafunzo jinsi ya kusajili na kutambua taarifa za awali za Wanafunzi, wazazi watapatiwa fomu za maombi kupitia watoto hao na baada ya kuzijaza kikamilifu zitarejeshwa shuleni tayari kwa kuhakikiwa na kuandaliwa vyeti.

Baada ya kujiridhisha pasipo shaka maombi yote yatatakiwa kulipiwa ada stahiki kupitia mfumo wa malipo wa Serikali na kisha vyeti vitaandaliwa na kurejeshwa shuleni tayari kwa kuwagawia Wanafunzi.

Zoezi hili  ni endelevu kwa Wilaya zingine na Mikoa yote Tanzania Bara.