Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Usajili wa Vizazi

Usajili wa vizazi unasimamiwa na sheria ya uandikishaji vizazi na vifo,(sura 108 toleo la 2002)

Kulingana na sheria kizazi inatakiwa kuandikishwa ndani ya siku 90 tangu kutokea kwake na kifo ndani ya siku30,na Tukio hilo Lazima liwe limetokea ndani ya mipaka ya Tanzania Bara.Pamoja na takwa hili sheria inaruhusu usajili kufanyika nje ya muda huu.Wajibu wa kusajili kizazi ni kama ufuatao:

NB: Baba au Mama,na kama Baba na Mama hawapo,mmiliki wa nyumba ambaye ana taarifa za kizazi kutokea,mtu yoyote ambaye amekuwapo wakati kizazi kikitokea au mtu yoyote ambaye mtoto aliyezaliwa yuko katika himaya yake.

 

UTARATIBU WA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA

1: Usajili wa kizazi ndani ya siku 90

 • Kama kizazi kimetokea hospitalini,kituo cha afya au zahanati hakikisha unapatiwa Tangazo la kizazi kabla ya kuondoka.
 • Endapo kizazi kitakuwa kimetokea nyumbani,toa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa kijiji au Msajili wa vizazi au vifo wa wilaya ili ipatiwe tanzazo la kizazi.taarifa hii itolewe ndani ya siku 90.
 • Wasilisha tangazo la kizazi kwa msajili wa vizazi na vifo wa wilaya kilipotokea kizazi
 • Lipa ada ya cheti inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 3500/=).

 

2: Usajili nje ya siku 90 lakini chini ya miaka 10.

 • Jaza na wasilisha Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3  (ijazwe na mzazi au mlezi)
 • Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
 • Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono maelezo yako kwenye fomu.nyaraka hizi ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
 • Lipia ada inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 4000/=) kwa wilayani na shilingi elfu 14,000/= kwa makao makuu

3: Kuandikisha kizazi kilichochelewa kuandikishwa zaidi ya miaka 10

 • Jaza na wasilisha  Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3 (ijazwe na mzazi au mlezi).
 • Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
 • Ambatanisha nyaraka ,kadi ya kliniki ya mtoto,cheti cha ubatizo kamakipo,barua kutoka mamlaka ya serikali zinazohusika kama vile ofisi ya mtendaji kata au kijiji),cheti cha kumaliza elimu ya msingi, cheti cha kumaliza elimu ya sekondari  kuthibitisha tarehe ya kuzaliwa,mahali pa kuzaliwa na uraia wa wazazi.
 • Kwa watu walio zaliwa zamani sana unapaswa kuwa na viambatanisho viwili ambapo utatakiwa kuwa na kadi ya utaifa pamoja naya kura au bima ya afya, kama mwombaji anataka kutumia kadi ya leseni ya gari lazima iambatane pamoja na kadi ya utaifa au ya kura.
 • Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tshs 10,000/=) kwa wilayani na shilingi 20,000/= kwa makao makuu.

4: Kupata nakala ya cheti baada ya kupoteza.

 • Wasilisha ombi lako ukionesha namba ya ingizo jina la mwenye cheti,mahali pa kuzaliwa na tarehe ya

           kusajiliwa.

 • Jaza taarifa zako katika Fomu ya kutafutia kumbukumbu (search form)
 • Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tsh.3500/= ikiwa Tshs.1500/= ada ya upekuzi na Tsh 2000/= ada ya makala ya cheti.

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa

 • Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa
 • Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako – barua inayotetea ombi lako na kiambatanisho(cheti cha ubatizo,kadi ya clinic au vyeti vya shule na vielelezo vingine msajili atakavyohitaji kwaajili ya kujiridhisha, vielelezo vya wazazi kama vile cheti cha kuzaliwa, vyeti vya vifo au vitambulisho vyao  ikiwa jina la mmoja wa wazazi limekoseewa)
 • Rejesha cheti kinachotakiwa kusahihishwa.
 • Ada baada ya ombi lako kukubaliwa (ada ya sasa ni Tsh6500/=(ikiwa ni:-3000/= ada ya kusahihisha , 1500/= ada ya upekuzi na 2000/= ada ya cheti)

 

Utaratibu wa kusajili na kupata cheti cha kifo

·                     Kwa vifo vya majumbani msimamizi wa mirathi atatakiwa kuwa na muhtasari wa wanandugu                           unaomteua kuwa msimazi ambao lazima upitie kwa mtendaji wa kata kwa ajili ya kuidhinishwa pamoja           na barua ya mtendaji wa kata.

                Ada ni shs.14,000/= ndani ya miaka 10 na shs.20,000/= zaidi ya miaka kumi kwa makao makuu na               wilayani  ni shs 4,000/= ndani ya miaka kumi na shs.10,000/= zaidi ya miaka 10

·                     Kwa vifo vya majumbani  kama marehemu yuko ndani ya siku 30 afike katika wilaya husika kwaajili ya           kusajili akiwa na vielelezo tajwa hapo juu. Ada ni shs 14,000/= kwa makao makuu na wilayani ni                     4,000/=

·                    Kwa vifo vya hospitalini ndugu wa marehemu hupewa kibali cha mazishi katika hospitali husika hivyo             basi aje nacho wilaya husika au makao makuu kwaajili ya kupata cheti cha kifo. Ada yake ni shs.3500

 

·                     Form mpya ya BD 6 iwekwe kwaajili ya kupakuliwa na wateja.

TANBIHI

 1. Kubadili au kuongeza jina.
  Sheria inaruhusu kubadili au kuongeza jina ndani ya miaka miwili tangu tarehe ya kusajiliwa.Baada ya muda huu kupita daftari la kizazi haliwezi kurekebishwa kwa badiliko la jina,mhusika atatakiwa kufuata utaratibu mwingine chini ya sheria ya kubadili jina kwa ajili ya (Deed polls).
 2. Taratibu mpya za kupata vyeti vya kuzaliwa kwa walio nje ya nchi.soma zaidi

>>> MASWALI MBALI MBALI YANAULIZWA KUHUSU VIZAZI


PROGRAMU YA USAJILI WA VIFO NDANI YA SIKU 30

Uandikishaji wa vifo ni mojawapo ya shughuli zinazofanywa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kutumia Sheria ya Uandikishaji wa Vizazi na Vifo sura ya 108.

Sheria imeanisha kuanzia kuanzia mwaka 2009 kuwa usajili wa matukio muhimu ya vizazi na vifo ni lazima kwa kila mtu.Hata hivyo miundombinu ya usajili iliyopo si rafiki katika kuhakikisha kuwa kila tukio linasajiliwa. Kwakuzingatia hayo serikali imekusudia; kusogeza huduma za usajili karibu na wananchi, kupunguza gharama kwa wananchi katika upatikanaji wa huduma za usajili na kuhakikisha taarifa na takwimu za matukio ya vifo zinapatikana kwa wakati.

Ili kufanikisha shughuli za usajili na utoaji vyeti vya vifo Wakala wa Usajili Ufilisi za udhamini (RITA) umezindua mpango mkakati wa usajili wa Vifo ndani ya siku 30 katika mkoa wa Iringa.

UTARATIBU WA KUSAJILI KIFO NDANI YA SIKU 30

Iwapo kifo kimetokea katika kituo cha tiba (hospitalini,kituo cha afya au zahanati) mhusika wa kituo cha tiba ( ambaye ndiye Msajili Msaidizi) wa kituo cha tiba anawajibika kuhakikisha taarifa za usajili wa kifo zimejazwa kwenye fomu ya usajili na kujaza cheti cha kifo.

Iwapo kifo kimetokea nyumbani au mahali pengine mwombaji atoe taarifa za tukio la kifo kwa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa  ambaye atajaza fomu maalum ya taarifa (notification) na kuwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kata. Mtendaji wa Kata ndiye atakayehusika kutoa cheti cha kifo kilicho andikwa kwa mkono kama uthibitisho wa Usajili wa kifo kilichotokea katika kata yake.

Cheti hiki kinatolewa bure, endapo cheti hiki kitapotezwa na mwombaji atahitaji nakala nyingine atawajibika kwenda katika halmashauri ambayo cheti hiki kilipatikana kulipia ada ya shilingi elfu 5000/=

 

MUHIMU: Usajili ufanyike ndani ya siku 30 tangu kifo kutokea.