Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Usajili wa Kizazi

Usajili wa vizazi unasimamiwa na sheria ya uandikishaji vizazi na vifo,(sura 108 toleo la 2002)

Kulingana na sheria kizazi inatakiwa kuandikishwa ndani ya siku 90 tangu kutokea kwake na kifo ndani ya siku30,na Tukio hilo Lazima liwe limetokea ndani ya mipaka ya Tanzania Bara.Pamoja na takwa hili sheria inaruhusu usajili kufanyika nje ya muda huu.Wajibu wa kusajili kizazi ni kama ufuatao:

NB: Baba au Mama,na kama Baba na Mama hawapo,mmiliki wa nyumba ambaye ana taarifa za kizazi kutokea,mtu yoyote ambaye amekuwapo wakati kizazi kikitokea au mtu yoyote ambaye mtoto aliyezaliwa yuko katika himaya yake.

UTARATIBU WA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA

1: Usajili wa kizazi ndani ya siku 90

 • Kama kizazi kimetokea hospitalini,kituo cha afya au zahanati hakikisha unapatiwa Tangazo la kizazi kabla ya kuondoka.
 • Endapo kizazi kitakuwa kimetokea nyumbani,toa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa kijiji au Msajili wa kizazi au vifo wa wilaya ili ipatiwe tanzazo la kizazi.taarifa hii itolewe ndani ya siku 90.
 • Wasilisha tangazo la kizazi kwa msajili wa kizazi na vifo wa wilaya kilipotokea kizazi
 • Lipa ada ya cheti inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 3500/=).


2: Usajili nje ya siku 90 lakini chini ya miaka 10.

 • Jaza na wasilisha fomu BD15 (ijazwe na mzazi au mlezi)
 • Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
 • Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono maelezo yako kwenye fomu.nyaraka hizi ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
 • Lipia ada inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 4000/=)

3: Kuandikisha kizazi kilichochelewa kuandikishwa zaidi ya miaka 10

 • Jaza na wasilisha fomu BD15 (ijazwe na mzazi au mlezi).
 • Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
 • Ambatanisha nyaraka ,kadi ya kliniki ya mtoto,cheti cha ubatizo kamakipo,barua kutoka mamlaka ya serikali zinazohusika kama vile ofisi ya mtendaji kata au kijiji),cheti cha kuthibitisha tarehe ya kuzaliwa,mahali pa kuzaliwa na uraia wa wazazi.
 • Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tshs 10,000/=).

4: Kupata makala ya cheti baada ya kupoteza .

 • Wasilisha ombi lako ukionyesha namba ya ingizo ,jina la mwenye cheti,mahali pa kuzaliwa na tarehe ya kusajiliwa.
 • Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tsh.3500/= ikiwa Tshs.1500/= ada ya upekuzi na Tsh 2000/= ada ya makala ya cheti.

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa

 • Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa
 • Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako – barua inayotetea ombi lako na kiambatanisho(kitambulisho cha kura n.k)
 • Rejesha cheti kinachotakiwa kusahihishwa.
 • Ada baada ya ombi lako kukubaliwa (ada ya sasa ni Tsh6500/=(ikiwa ni:-3000/= ada ya kusahihisha , 1500/= ada ya upekuzi na 2000/= ada ya cheti)

TANBIHI

 1. Kubadili au kuongeza jina.
  Sheria inaruhusu kubadili au kuongeza jina ndani ya miaka miwili tangu tarehe ya kusajiliwa.Baada ya muda huu kupita daftari la kizazi haliwezi kurekebishwa kwa badiliko la jina,mhusika atatakiwa kufuata utaratibu mwingine chini ya sheria ya kubadili jina kwa ajili ya (Deed polls).
 2. Taratibu mpya za kupata vyeti vya kuzaliwa kwa walio nje ya nchi.soma zaidi

>>> MASWALI MBALI MBALI YANAULIZWA KUHUSU VIZAZI