RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
December
23
2025
Unknown
News & Update
`

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainabu  amewaasa wananchi  kutoa taarifa kwa Kabidhi Wasii Mkuu ambaye ndiye Mdhamini Umma kuhusu watoto walio chini ya umri wa miaka 18 ambao wameachiwa mali na kukosa  usimamizi mzuri au zenye viashiria vya migogoro na mali zisizokuwa na wenyewe au wamiliki kuwa na changamoto ya afya ya akili ili ziweze kusimamiwa kwa misingi ya kisheria na RITA.

Mhe. Katimba  ameyasema hayo wakati wa  hafla ya kumpongeza Bi. Anna Zambi ambaye ni  mnufaika wa huduma ya Udhamini wa Umma kwa kuhitimu Shahada ya kwanza ya Sheria katika chuo kikuu cha Tumaini tawi la Makumira leo Disemba 23, 2025 Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA  Bw. Frank Kanyusi amesema kwa sasa wamejipanga kuwafikia wananchi kule walipo kwa kuanzisha kliniki maalum zinazotembea (mobile Clinic) na kwamba timu ya wanasheria na wataalam wengine wa RITA watapokea na kutoa msaada kwa jamii kuhusu changamoto mbalimbali za kisheria hasa usimamizi wa mirathi na Ufhamini wa Umma.

"Wakala unaendelea  na mkakati wa kuboresha huduma na kuhakikisha upatikanaji mzuri kidigitali kwa kushirikiana na taasisi zingine za umma na binafsi". Alisema Bw. Kanyusi