RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
MEDIA CENTRE
August
26
2025
RITA YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA USTAWI WA JAMII
News & Update
`

Waziri wa Maendeleao ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima leo Agosti 26, 2025 ametembelea banda la Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwenye maadhimisho ya wiki ya Ustawi wa Jamii yanayoendelea katika viwanja vya chuo cha Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Gwajima ameipongeza Wakala kwa kutoa huduma bora kwa jamii na kuiomba kuendelea kuwahudumia kwa ukaribu watu wa makundi maalum. 

Wakala unaendelea kutoa elimu ya huduma ya kusajili na kupata cheti cha kuzaliwa na kifo, huduma ya ndoa na talaka pamoja na msaada wa kusheria bure kuhusu kuandika na kuhifadhi wosia.