Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua rasmi maonesho ya Teknolojia ya Madini leo Septemba 22, 2025 katika viwanja vya Samia Suluhu Hassan, Bombambili Mkoani Geita.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Kassim Majaliwa amezipongeza taasisi za serikali na wadau mbalimbali kwa ushiriki wao mpana katika maonesho hayo na mchango wao mkubwa wa ukuaji wa sekta ya madini nchini.
Aidha, Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella ametoa rai kwa Taasisi mbalimbali, wawekezaji na wananchi kwa ujumla kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika ukuaji wa sekta ya madini mkoani humo.
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) unashiriki maonesho hayo kwa kutoa huduma za usajili wa vizazi na vifo, elimu kuhusu kuandikana kuhifadhi wosia, usimamizi wa mirathi pamoja na usajili wa bodi za Wadhamini wa taasisi, asasi za kiraia, madhebebu ya dini na vilabu vya michezo.