Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainabu amewaasa wananchi kutoa taarifa kwa Kabidhi Wasii Mkuu ambaye ndiye Mdhamini Umma kuhusu watoto walio chini ya umri wa miaka 18 ambao wameachiwa mali na kukosa usimamizi mzuri au zenye viashiria vya migogoro na mali zisizokuwa na wenyewe au wamiliki kuwa na changamoto ya afya ya akili ili ziweze kusimamiwa kwa misingi ya kisheria na RITA.
Mhe. Katimba ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumpongeza Bi. Anna Zambi ambaye ni mnufaika wa huduma ya Udhamini wa Umma kwa kuhitimu Shahada ya kwanza ya Sheria katika chuo kikuu cha Tumaini tawi la Makumira leo Disemba 23, 2025 Jijini Dodoma.
Kwa upande wake Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi amesema kwa sasa wamejipanga kuwafikia wananchi kule walipo kwa kuanzisha kliniki maalum zinazotembea (mobile Clinic) na kwamba timu ya wanasheria na wataalam wengine wa RITA watapokea na kutoa msaada kwa jamii kuhusu changamoto mbalimbali za kisheria hasa usimamizi wa mirathi na Ufhamini wa Umma.
"Wakala unaendelea na mkakati wa kuboresha huduma na kuhakikisha upatikanaji mzuri kidigitali kwa kushirikiana na taasisi zingine za umma na binafsi". Alisema Bw. Kanyusi