Swahili   |   English
Vizazi & Vifo - Online Portal

KUPATA HUDUMA YA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) unapenda kuufahamisha Umma kwamba sasa unaweza kutuma maombi ya kupata huduma zifuatazo kwa njia ya mtandao:

  1. Maombi mapya ya usajili wa Vizazi na Vifo
  2. Kuhakiki cheti cha kizazi au Kifo 

Mambo muhimu ya kuzingatia unapofanya maombi:

  1. Tunza taarifa ulizotumia kufungua akaunti,
  2. Mwombaji awe na taarifa zake sahihi pamoja na wazazi wote wawili,
  3. Mwombaji atapata Ankara ya malipo na atatakiwa kulipa kwa njia ya Benki (NMB and CRDB) au Mitandao ya simu (M-PESA, TIGO PESA and AIRTEL Money) tu kwa mujibu wa maelezo utakayopewa.
  4. Mwombaji awe na nakala laini (soft copies) za viambatanisho vinavyotakiwa katika mfumo wa pdf,
  5. Mwombaji aainishe wilaya atakayochukulia cheti

Aidha, Tunapenda kuwasisitizia waombaji wote kufuata maelekezo hapo juu ili kuepuka usumbufu.

Anuani ya maombi ya e-Huduma pamoja na Mwongozo wa maombi ya huduma yanapatikana hapo chini ya ukurasa huu

Kumbuka: maombi hayatafanyiwa kazi kabla ya kukamilisha malipo ya ada ya huduma.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0800 117 482