RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
June
23
2025
WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA 2025
News & Update
`

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amefunga rasmi maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma leo Juni 23, 2025 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

Aidha Mhe. Majaliwa amezindua mifumo miwili ambayo ni mfumo wa kielekroniki unaowezesha mifumo ya serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa ujulikanao kama Government Enterprise service bus (GovESB) na mfumo wa pili ni wa e-Wekeza unaowezesha mtumishi wa umma kuwekeza katika mfuko wa faida (Faida Fund).

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe. George Simbachawene amewapongeza watumishi kwa kazi bora wanayofanya na kuwaomba wasiache kutoa changamoto yoyote inayojitokeza kwa viongozi wao. Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeshiriki katika maadhimisho hayo kwa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa, huduma ya elimu ya ndoa na talaka pamoja na huduma ya kuandika na kuhifadhi wosia.

Tags : #Tanzania