RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
August
28
2025
Unknown
News & Update
`

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na taasisi ya VITAL STRATEGY leo Agosti 28, 2025 wilayani Kibaha mkoani Pwani imekutana na wadau ili kujadiliana na kupata maoni kuelekea maandalizi ya Mpango Mkakati wa Usajili wa Matukio muhimu ya Binadamu kwa mwaka 2025/2026 - 2030/2031.

Akizungumza wakati wa kufungua  kikao hicho kwa niaba ya Naibu Kabidhi Wasii Mkuu Bi. Irene Lesulie, Mkurugenzi wa Ulinzi na Haki za Kisheria Bw. Francis Kugesha amebainisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana  kupitia Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu wa mwaka 2015/ 2016 - 2020/2021 ambayo ni pamoja na kufanya maboresho ya Sheria ya vizazi na vifo na kuwezesha kugatua majukumu  ya usajili wa vizazi na vifo kufanyika katika vituo ya afya ya uzazi mama, baba na mtoto na ofisi za watendaji kata.

Bw. Kugesha kuwa mafanikio mengine ni kuimarishwa kwa matumizi ya TEHAMA ambapo kwa sasa mwananchi anaweza kutuma maomba ya usajili wa vizazi na vifo popole alipo kidijitali kupitia mfumo wa eRITA, kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za umma, binafsi, mashirika na wadau wa maendeleo.