RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametembelea banda la Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwenye maonesho ya kimataifa ya kibiashara (Sabasaba) leo Julai 11, 2025 Jijini Dar Es Salaam.
Dkt. Ndumbaro ameiopongeza RITA kwa kazi nzuri inayofanyika kwa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa papo hapo huku akiwahimiza wananchi kuendelea kujisajili kidijitali kupitia eRITA kwa kutumia simu zao au kompyuta popote walipo hata baada ya kumalizika kwa maonesho hayo.
Wakala unaendelea kutoa elimu kuhusu huduma zake mbalimbali pamoja na kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kuandika na kuhifadhi wosia.